STAA wa Shindano la Big Brother, Mwisho
Mwampamba, amesikitishwa na vitendo vya ubaguzi alivyofanyiwa na Polisi
wa nchini Namibia, anakoishi na mkewe, Meryl Shikwambane, ambapo
walimfuata kwenye nyumba yake na kumtaka aondoke nchini humo.
Mwisho ameandika kwenye ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa Facebook, akisema nchi hiyo sasa hivi imekuwa kama
Afrika Kusini, ambako wageni, hasa wenye ngozi ya Kiafrika, hupata
shida ya kuishi kutokana na kubaguliwa.
“Mimi nimeoa mtu wao na nimezaa naye
mtoto, nashangaa kubaguliwa na polisi hao, pia inashangaza kuona
wakiwahudumia vyema wageni kutoka barani Ulaya, lakini sisi Waafrika
wenzao tunabaguliwa,” alisema Mwampamba.
Mkali huyo ameshangazwa kupewa hati ya
kuishi nchini humo kwa miezi miwili pekee, wakati ameoa mwanamke wa nchi
hiyo, huku akipata shida hiyo hata mipakani
No comments:
Post a Comment