14 September 2013

Recho ........"Namshukuru mungu sina ukimwi"

Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ amejikuta akivuja jasho la furaha baada ya kupima Ukimwi na kujikuta yupo salama.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Sinza Palestina ambapo Recho alienda kupima katika Hospitali ya Amen iliyopo Sinza ambapo kabla hajapata majibu hayo alikuwa akihaha huku na kule kutokana na wasiwasi.

Baada ya vipimo hivyo, Recho alipewa majibu yaliyoonesha kuwa yupo salama kitu ambacho kilimsababisha acheke na kuwataka wenye wivu wajinyonge.

“Namshukuru Mungu kwa sababu nimejikuta mzima baada ya kupima UKIMWI, Mwenye wivu na maisha yangu ajinyonge tu,” alisema Recho.




No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname