Aisha Bui.
HUKU
kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na
kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na
kufafanua juu ya tuhuma hizo.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya
simu kutokea Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati
yeye yuko nchini humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake
hakuwa tayari kulianika.
“Jamani hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu. “

No comments:
Post a Comment