Binti wa umri wa miaka 15
tunayemtambulisha kwa jina moja tu la Zaina, mkazi wa Kimara jijini Dar
ameamua kufunguka na kusimulia jinsi alivyokuwa akibakwa na baba yake
mzazi aliyemtaja kwa jina moja la Mohamed.
ANAANZA KWA KUANIKA HISTORIA YAKE FUPI!
Akisimulia kwa uchungu, Zaina alianza
kwa kuanika historia yake kwa ufupi kwamba tangu atoke tumboni, hakuwahi
kumuona mama yake zaidi ya kuoneshwa kwenye picha tu!
Akasema hiyo yote ilitokana na hadithi
aliyowahi kusimuliwa kwamba, akiwa kichanga, baba huyo alimuiba kwa mama
yake anayeishi Kigamboni, Dar na kwenda kumlea Kimara kwa ushirikiano
na mama yake wa kufikia.
Lakini akasema: Hata huyo mama wa kambo
mwaka jana aliachana na baba baada ya kutufumania chumbani mimi na baba,
akakasirika na kuondoka zake.
SIKIA FILAMU KAMILI SASA
“Nakumbuka ilikuwa mwanzoni mwa mwaka
jana, nikiwa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kimara ndipo baba
alipoanza tabia ya kunilazimisha tufanye mapenzi. Alisema anataka
tufanye kwa njia ya kawaida na ya kinyume na maumbile.
“Nilikataa lakini akawa ananilazimisha
na vitisho juu. Tulianza kwa kufanya mchezo huo na baba lakini si kwa
kupenda kwangu, nililazimika kwa sababu niliamini ni baba ambaye anaweza
kunifanya lolote kama nitakataa, mbaya zaidi hakuwa akitumia kinga,”
alisema na kuongeza:
“Kuanzia hapo, zoezi hilo liliendelea
kila siku hadi mwishoni mwa mwaka jana nilipoamua kutoroka na kwenda
kuwaeleza ndugu wa baba, kule Tanga.”
Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa
kusema kuwa, kilichomsukuma kutoroka ni mateso, ukatili na
udhalilishwaji uliopitiliza kwani baba yake wakati akimwingilia alikuwa
akimkaba kooni ili asipige kelele.
“Yeye alijua anafanya kosa, akawa
akiniingilia huku ananikaba koo nisipige kelele. Nilikuwa nasikia
maumivu makali balaa,” alisema binti huyo.
ALIWAAMBIA MAJIRANI LAKINI WALIOGOPA KUMVAA BABAKE
“Kingine kilichonifanya nitorokee Tanga
kuwaambia ndugu zake ni kwamba, niliwahi kuwaambia majirani kuhusu
mchezo wa baba lakini hakuna aliyethubutu kumuuliza kwa vile
wanamuogopa,” alisema.
MAMA MZAA BABA AAMBIWA KILA KITU
Zaina alizidi kusema kuwa, baada ya kufika Tanga alimweleza kila kitu bibi yake (mama mzaa baba’ke).
Bibi huyo kwa sababu ni mzazi alimwita
mwanaye na kumkanya kisha akafanyiwa mambo ya kimila ili kuondoa balaa
hilo la baba mtu kutembea na mwanaye wa kumzaa la sivyo kwa mila za kwao
ukoo mzima ungesambaratika.
BABA MTU AONDOKA TANGA USO UMEMSHUKA, YEYE AGOMA
“Baada kufanyiwa mambo ya mila, baba
aliniambia turudi Dar lakini nilikataa kwa sababu niliamini tutakapofika
bado atataka kuniingilia tena. Nasema hivyo kwa sababu pia baba amewahi
kufanya mapenzi na dada’angu anaitwa Hamida mpaka akampa mimba.
“Huo ukatili wote alikuwa akitufanyia
kwa nyakati tofauti tofauti, dada alipopata mimba siku moja alimwibia
fedha ili akaitoe, alifanikiwa na akakimbia nyumbani, sijui alipo,”
alisema.
Akaendelea: Basi, niliamua kubaki kwa
bibi, lakini kuna siku alikuja mtu aliyekuwa anatafuta msichana wa kazi
‘hausigeli’, mimi nikakubali, nikaenda Moshi ambako nilikaa kwa muda.
Inatoka Uk. 2
“Hivi karibuni nilirudi Dar na kufikia
kwa jirani, sikutaka kwenda nyumbani kwa baba, namuogopa atataka tena.
Huyu jirani niliyefikia kwake, mtoto wake ni rafiki yangu tulikuwa
tunasoma naye. Hapa nilipo natafuta msaada wa kumpata mama yangu mzazi.
Kama atabahatika kulisoma gazeti hili namuomba anifuate jirani na kwa
baba atanipata,” alisema Zainab.
Zainab hakuishia kwenye kufikia kwa
jirani tu, anasema akiwa hapo jirani huyo kesho yake alimpeleka serikali
za mitaa ili kutoa taarifa kuwa amerudi kwa vile alitafutwa kwa muda
mrefu kwenye shule aliyokuwa akisoma.
MWENYEKITI WA MTAA AKIRI ZAINAB KUBAKWA NA BABA’KE
Naye mwenyekiti wa mtaa wa eneo hilo,
Demetrius alikiri kumpokea mtoto huyo na kumsimulia yote kuhusu baba
yake ambapo aliambatana naye hadi Kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusuf kwa
lengo la kutoa taarifa ili mzee huyo achukuliwe hatua za kisheria.
Alisema binti huyo alifunguliwa jalada la kesi KMR/RB/114/2013
UCHUNGUZI.
BABA ANASEMAJE?
Baada ya kumalizana na binti huyo
aliyeungwa mkono na mwenyekiti huyo, mapaparazi wetu walizungumza na
baba mtuhumiwa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Si kweli, huyo mtoto ananisingizia tu, mimi siwezi kufanya kitu kama hicho na binti yangu wa kumzaa hata siku moja.
-Gazeti la Ijumaa via GPL
No comments:
Post a Comment