31 August 2013

RAY C AHAHA KUPUNGUZA UNENE..!!

Hakika sexy lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amepona na sasa anahaha kukata minyama uzembe baada ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’. Ray C au Kiuno Bila Mfupa, juzikati alitupia picha kwenye ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa Instagram zikimuonesha akiwa ‘bize gym’ akifanya mazoezi makali kupunguza unene akijiandaa kurejea rasmi kwenye gemu. Picha hizo zinamuonesha akikimbia kwenye mashine maalum ya kukimbilia, akifanya mazoezi ya viungo na nyingine akifanya mazoezi ya kukata tumbo ambapo mashabiki wake kwa asilimia kubwa walimpongeza kwa hatua hiyo. “Kiuno Bila Mfupa umetishaaa…sasa umerudi enzi zile…bora ulivyoamua kufanya mazoezi,” yalisomeka sehemu ya maoni hayo.
Baada ya kupona na kuacha madawa ya kulevya kwa msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete baada ya kutolewa kwenye magazeti ya Global akiwa hoi, sasa anasubiriwa kwa shauku na mashabiki wake wanaotamani kumuona stejini kwa mara nyingine.
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni lilipokea ‘nyiuzi’ kuwa Septemba 29, mwaka huu (Alhamisi) iliyopita, Ray C alibatizwa kwa maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Bunju, Dar

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname