Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na
familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza
litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’. Msuya
aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku familia ikitangaza
kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake wamemwachia Mungu.
Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza
lililobeba mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagizwa Nairobi, la aina
yake huku likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni
ya Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza
kifaa maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.
Hali hiyo ilionekana kuwaacha na
mshangao maelfu ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada
iliyofanyika nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa
kumiminiwa risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo
nyumbani kwao eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani
Manyara.
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema
jana kuwa mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria
Msuya ‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.
Source:Jamii forums

No comments:
Post a Comment