07 August 2013

BONGO STAR SEARCH SASA NI NDANI YA TBC1 NA SI ITV KAMA ZAMANI, NA HIZI NDIZO SABABU ZA KUHAMIA TBC1



Bencmark Productio CEO Madam Rita Paulsen
Madamu Rita wa Epiq Bongo Star Search kaelezea sababu zilizofanya kipindi chake hicho kuanza kurushwa na TBC1 jumapili hiina isiwe ITV kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma..
Katika mtandao wa FaceBook ktk Page yake ameandika maneno yafuatayo..
""Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1.

Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving'amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.

Nashukuru sana kwa maoni yenu mlioyatoa na mmesikika. Nawatakieni siku njema!""

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname