06 July 2013

MJUE MZEE ABDULLAH ALRUWEIHY ALIYETEMBEA KWA MGUU KUTOKA DAR HADI TANGA.


Mwarabu aliyetembea kwa Miguu Dar es salaam mpaka Tanga.
Baba yake alitembea kutoka Dar es salaam mpaka  Kigoma
Yafuatayo ni mahojiano yaliyofanyika kati ya mwandishi  na mzee Abdullah Mohammed Alruweihy mwaka 2007 katika kijiji cha Saadani eneo la Tongoni wakati  wa uhai wake.Alifariki mwaka 2009/2010.Mwenyezi Mungu amrehemu.
Swali:Sisi pale jijini Tanga tunakufahamu zaidi kwa jina la mzee Ruwehi.Jina lako kwa ukamilifu ni nan?.
Jibu:Mimi jina langu ni Abdullah bin Muhammad bin Habiib bin Salim bin Ally bin Suleiman bin Salim Al Rawaahy.
Swali:Umezaliwa wapi?.
Jibu:Nimezaliwa kijiji cha Ndono kwa Mwana Kurwa  Tabora.
Swali:Tupe historia ya wazazi wako kwa kifupi.
Jibu:Mama yangu  alikuwa akiitwa  Zuhura kutoka kabila la Manyema.Baba yangu alikuwa ni mmoja ya wafanyaji wa biashara aliyetoka kutoka nchi ya Oman.Alikuja mpaka Zanzibar.Akaona Zanzibar hapamfai akaondoka kuelekea sehemu za bara.Akafika sehemu moja inaitwa Tabora kama nilikutajia.
Sasa baada ya kufika hapo.Huyu bwana alikuwa anafanza kazi za biashara.Wakati huo walimchunuka Majarumani.Na ikawa wanatumia vitu vingi  katika dukani kwake.
Sasa  ilipokuwa imetokea ile vita wak
awa majarumani wanashambuliwa na waiengereza.
Swali:Ni vita gani hiyo?
Jibu:Ni vita ya 1914
Swali:Jee ndiyo ile vita ya mwanzo ya dunia?.
Jibu:Hapana,haikuwa vita ya mwanzo ya dunia.Ile vita ya maji maji ni vita mbali ile.Hii ilikuwa ni vita ya pili.
Swali:Ilikuwa ni mwaka gani?.
Jibu:Ilikuwa ni  1914.
Swali:Wewe ulizaliwa mwaka gani hasa?.
Jibu:Mimi nilizaliwa tarehe 10/02/1908
Swali:Tuendelee na historia ya wazazi wako.
Jibu:Mzazi  wangu mbali na kufanza utaratibu akawa na mlahaka na wale wajarumani mpaka ilipoingia vita.
Vita iliendelea mpaka baadae akaja mmoja anaitwa bwana Robert Fonreto. Akamwambia Muhammed una habari?.Vita inaendelea vikali na sisi hapa tulipo hatukukaa vizuri.Akamwambia sasa tutafanza nini?.Akamwambia risasi imekuwa kidogo na baruti  kidogo lakini askari wapo wa kuweza kuendesha kazi.Sasa tutafanza mashauri  gani?.
Akamwambia kama shauri ya risasi na baruti mimi nitafanza taratibu ya kuweza kutafuta na maarif mengine.Akamwambia unaweza  kweli,akajibu ndio.Akamwambia haya ondoka nenda.
Akaondoka moja kwa moja mpaka akafika Dar es salaam.Wakati ule wajarumani wenyewe ndio wameikamata Dar es salaam.Akatoka Dar es salaam moja kwa moja mpaka akafika kwenye nchi ya Mukkalla,Yemen.Akatoka Mukalla akenda juu,akapata risasi na baruti jumla debe thamanini na nne (84).
Ikawa chini akaweka risasi na madebe mengine akaweka baruti,lakini juu akaweka tende.Akaajiri jahazi moja lakini mimi wakati ule bado mdogo.Lakini ile historia walivyokuwa  wananieleza wale waliiokuwa wenziwe.
Akasikilizana na nahodha kuwa hii ni tende nipelekee Dar es salaam.Nahodha akaondoka mpaka akafika Unguja.Wakati ule Unguja ilikuwa ndani ya mikono ya waarabu wenyewe.Unguja ana nduguze.Mmoja anaitwa sheikh Suleiman bin Said Alruwahiy.Anakaa sehemu moja kule Unguja panaitwa Michungwa miwili.
Walipofika kule wakamwambia habari gani uliyonayo Mohammed?.Aliwaambia sina habari yoyote.Nimekuja tu kuwasalimia.Hakuwaambia ile siri yake.
 Ile jahazi baada ya pale akamwambia chukua hii mizigo kateremshe Dari salaam.Mimi nipo kidogo hapa halafu nakuja.Nahodha akaendesha jahazi hadi Dari salaam.Wakati ule ilipofika ile jahazi Dari salaam haipo tena ndani ya mikono ya Wajarumani.Imo ndani ya mikono ya Muiengereza.Kashatawala muiengereza.     ITAENDELEA...
CHANZO  http://www.islamictides.com

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname