Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva ambaye anafanya Vizuri sana na Stayle yake ya Bongo Bolingo Hamisi Ramadhani Muite H-BABA.
Ameamua kutoa kauli yake juu ya swala zima la Kufuturisha ambalo
limechukua nafasi katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,
H-Baba ameamua kutoa kauli hiyo baada ya kuona watu wanafanya mambo hayo kinyume na Taratibu za Misingi ya Dini,
"Nawapongeza
kwa wale wanaoenda kufuturisha watoto Yatima na waendao kufuturisha
Misikitini nawapa pongezi sana kwasababu wanapata dhawabu kubwa sana
kuliko wale wanaoalika watu wasioeleweka majumbani kwao alfu
wanafuturisha alfu usifanye hivyo kutaka sifa unawaita wandishi wa
habari nyumbani kwako ili watu wajue, inakuwa siyo swala la msingi.
Sisi
watoto wa kiislamu sifa na Mwezi wa Ramadhani ni vitu viwili tofauti
tusitake sifa kuonekana wasafi au kuonekana Bora katika kipindi hiki,
inabidi sisi wote turudi nyuma na kuacha maovu yetu yote tulikua
tukifanya, kama unafanya jambo lako nenda msikitini utawakuta watu
ambao wako pale kwa ajili ya swala toa msaada wako pale au futurisha
pale, Utapata dhawabu kubwa sana.
Lakini
uanapokuwa nyumbani kwako ukaalika wasanii wenzako watakuja lakini
kumbuka wengine hawajafunga, mwingine katoka bar, Mwingine kasuka,
Mwingine kavaa Heleni mwingine kavaa hiki na hiki haiswii kwa sisi
watoto wa Kiislamu, Tusitake sifa sisi wasanii tumekuwa wataka sifa.
Leo
umesikia Flani kafuturisha eti na wewe kesho yake unaamka na mimi
nafuturisha jamani tusifanye kama kamchezo huu ni mwezi wa Ramadhani
tuache sifa, Mimi mbona nimefuturisha nani anae jua?
kufuturisha ni wewe na ndugu zako na marafikizako wa karibu, siyo leo
nafuturisha Mwandishi Flan Njoo unipige picha njoo unimulike Watanzania
waone, wewe ndugu yangu mambo hayaendi ivyoo bwana haiswii maana lazima
tambiane ukweli unapofanya jambo baya mwezi huu wa ramadhaniKwanza
wewe Mtoto wa kiume Haujaoa unalala na mwanamke haujamuoa je inaswii..?
pia mtoto wa kike unalala na mwanamume hajakuoa je inaswii..? jamani
tusichezee Dini hiki siyo kipindi cha kufanya mabo yetu kutafuta
sifa,huu ni muda wa kutubu, muda wa kumrudia mola pia ni muda wa
kujisafisha.
Me
nimeoa mke wangu ananipikia ftari vizuri nafunga na mpaka kwa sasa
kishavu kinatoka,Nafuturisha watu wanakuja kwangu wanafuturu lakini siyo
kwa sifa sasa mnaita mpka TV, Magazeti na Redio aaah jamani nani wewe?
sifa za nini kipindi hiki ? unatubu nini sasa? jamani wasanii wenzangu
nawasii tuache sifa namaliza kwa kusema KWA ALLAH HAKUNA SIFA" alisema H-BABA
Unaweza kuona Video H-BABA akiwa anaongea...
ALICHOSEMA H BABA NAMUUNGA MKONO .KWANI KAKA ZANGU AU WANAWAE WENZANGU WANAONA SIFA KUFUTURISHA ILA MAANA YA KUFUTURISHA HAWAIJUI . KWANI UTAKUTA WANAOISHI KIMADA WAPO WASOFUNGA WAPO SASA SIMNGEPELEKA WATOTO YATIMA WAKAFURAHIE FUTARI .
ReplyDeleteSIFA TU