katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu
KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule
ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha
shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa
anajihusisha na imani za Kishirikina.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina
Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi
wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata
taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa
hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na
kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo
akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema
tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke
shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi
aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na
baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na
uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka
Shuleni hapo baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya
anakoishi na Binamu yake.
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the
SameSun iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari
kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule
ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne
Mwakani.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood
Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo
na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka
kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili
ahamie.
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya,
Wiliamu Simwale alisema alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama
lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo
Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa
taarifa kwenye shirika linalolipa.
Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under
the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na
tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili
umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine
zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment