Picha aliyoweka Wema Sepetu Instagram kuelezea ugomvi uliotokea, na
kuandika: ” Da fight I got into today caused me da marks I hav on my
baq… things I do for da people I love always cost me… nd u knw wat ama
kip doin.”
Staa huyo wa Bongo Movie ambaye pia ni mmilikiwa kampuni ya
Endless
film, amemfikisha mama yake mzazi anayejulikana kama Miriam Sepetu
kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama jijini Dar es salaam kwa madai ya
kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa
samani ndani ya nyumba yake.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.
“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na
kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi
ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,”
Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada
mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye
jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

No comments:
Post a Comment