Huyu ni Omar Borkan Al Gala, mwigizaji na pia mpiga picha wa huko
Dubai ambaye kwa mujibu wa taarifa, yeye pamoja na wenzake wawili
wamefukuzwa huko Saudi Arabia kutokana na kuwa na muonekano mzuri
kupitiliza
(Yaani ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.
Omar alitolewa na maafisa wa polisi na kunyimwa kuhudhuria katika
tamasha ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo ambalo huusisha mbio za
Ngamia, Janadriyah Festival ambalo kwa sehemu kubwa huhudhuriwa na
matajiri, na baadhi ya vyanzo vya taarifa vinasema Omar alitolewa
kutokana na mualiko wa msanii wa kike maaruku kutoka Falme za Kiarabu
ambaye walihofia angeweza kutengeneza mahusiano naye.... na wengine
wakisema ni hofu ya wakubwa kuibiwa mademu wao.
(Yaani ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.
CHANZO : SAM MISAGOBLOG
No comments:
Post a Comment