Watu wanaosadikika kuwa ni wahuni wa kitechnolojia wameonekana
kutenda mambo yao katika Official website ya Daddy wa muziki wa rap
Tanzania, Proffesa Jay http://www.professorjaytz.com/.. ambayo
kwa mujibu wake mwenyewe, site hii ilikuwa bado ipo katika matengenezo
na kuna mtu maalum ambaye alikuwa amemuasign kazi ya kuitengeneza.
![]() |
| Hivi ndivyo site ya msanii huyu inavyoonekana kwa sasa; |
Jay mwenyewe ambaye hadi wakati tuliokuwa tunaongea naye alikuwa
hafahamu kuhusiana na kutokea kwa issue hii, amewaahidi
mashabiki wake
kulifuatilia swala hili na kuhakikisha anaweka kila kitu katika mstari.Rapa huyu mchana wa leo atakuwa akitoa Burudani pande za Chuo kikuu Cha Dar es Salaam katika Kongamano maarufu la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere kwa mwaka huu, Kongamano ambalo limeanza jana na linatarajiwa kuisha siku ya kesho likiwa na kauli mbiu 'Maendeleo ni Mapambano ya Ukombozi'.
CREDIT -SAMMISAGO

No comments:
Post a Comment