Amana Mbijili 30 mkazi wa Vinhawe Wilayani Mpwapwa akiwa haamini Baada ya
kuambiwa Mtoto aliyejifungua Kafariki, kama alivyokutwa na Mpiga picha
wetu Katika wodi Namba 17
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la kubadilishwa kwa
watoto mara baada ya wazazi wao kujifungua wachungulia madirishani
Kwenye whodi namba 17 jana
AMANA Mbijili Mkazi wa kijiji cha Vinhawe Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ameilalamikia Hospital ya Rufaa
ya General kwa kitendo cha manesi
kumbadirishia motto baada ya kujifungua.
kumbadirishia motto baada ya kujifungua.
Tukio hilo lililotokea jana Hospitalini Hapo majira ya saa
11 jioni baada ya Mwanamama Huyo kujifungua kwa njia ya upasuaji na moja kwa
moja kupelekwa chumba cha mapumziko kilizua Tafrani .
Akielezea tukio hilo Mbijili alisema alishangazwa na kitendo
cha yeye kulazwa chumba tofauti na mtoto wake ndipo alipo muuliza mmoja wa
manesi alipo mtoto wake akajibiwa kuwa mtoto huyo alishafariki kitendo
ambacho yeye hakuridhika nacho.
Alisema hakuridhika kutokana na kuona mtoto mwingine
akipitishwa na kuingizwa chumba kingine akiwa amefungwa moja ya nguo alizofika
nazo hosipitalini hapo akiwa hai ndipo akaanza kulalama na baada ya kuona hivyo
nesi yule akaenda kumletea mtoto akiwa hai na kumkabidhi.
Amana alisema‘’nilipoanza kulalamika kwa sauti ndipo wakaamua kuniletea
mtoto wangu akiwa hai kitendo kilichonifanya nilie kwa furaha baada ya kumpata
mwanangu, japo sijui kama walichanganya watoto au walitaka kuniibia makusudi
maana hata hivyo sikuona mama wa huyo marehemu mungu ndiye anajua mimi namshukuru,’’
alisema Amana
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Zainab Chaula alisema ni
kweli tukio hilo lilitokea lakini limenukuliwa tofauti maana yeye anachojua
Mama wa Mtoto huyo alifanyiwa upasuji baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya
kawaida.
Chaula alisema kawaida mtotoakizaliwa lazima alie lakini
mtoto huyo hakulia ndiyo sababu ya kumpeleka Chumba cha Leba kuliko na kitanda
chenye mashine maarumu na hata hivyo Mtoto huyo alifariki.
‘’ hiyo ya kupewa Mtoto akiwa hai ni uvumi usio na maana,
kwani baada ya kuona kelele zimezidi ikabidi tumwambie Baba wa mtoto kuwa amefariki na alidhibitisha kutokana na mtoto
kufanana nae na yule,’’ alisema
HABARI NI KWA HISANI YA JOHN BANDA
No comments:
Post a Comment