UJUMBE TOKA KWA MDAU...........
NAWAPA KISA KIFUPI TUU AMBACHO KINANISIBU KWA SASA,
Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia
yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara
ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko
tayari kukopa
mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna
sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni
kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume).
Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially
akina mama.
Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye,
naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi
miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa
akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani
nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa
ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela,
hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba
nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela
kubwa (30,000).
Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake
anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr.
atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake
akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole.
Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe
msaada.
Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa
anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa
nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba
alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo
kidogo hivyo hivyo.
Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna
kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote
niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale,
nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu
ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi
kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe
tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta
kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo.
ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu
message hizo.
Najua fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu
ni kuwa haya yote yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na
familia yake. Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na
hatumi hela kwa visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau,
naombeni comment zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the
situation. Sisemi kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna
wakati wa kupata na kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe
mwanaume fanya juu chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni
wako, lakini hawa wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia
majaribuni. Mimi sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya
mapenzi lakini mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani
alaumiwe?
No comments:
Post a Comment