Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Majani ya Chai
iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam, wametajwa kujiingiza katika kashfa
ya ngono, kuvuta na kuuza bangi katika moja ya nyumba zinazozunguka
shule hiyo,
gazeti la mwananchi linaripoti
Hilo
ni tukio lingine jipya, kwani mwishoni mwa mwaka jana, kuliibuka
matukio ya ajabu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi, Ruaruke, Rufiji
mkoani Pwani ambao walielezwa kujihusisha na uvutaji bangi hata
kukonyeza na kubaka walimu wao.
Mkuu wa Sekondari hiyo, Jasinta Assey(Pichani juu) alikiri na kusema kwamba vitendo vya uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake, vinachangiwa na askari wa Kituo kidogo cha Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa kwa wauzaji wa bangi na nyumba bubu za wageni. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Shule hiyo, Jasinta Assey alisema ni kawaida ya polisi hao kwenda kwenye nyumba hizo kunakofanyika biashara hizo na kuchukua rushwa badala ya kutatua tatizo.
No comments:
Post a Comment