Matumaini (katikati) akisaidiwa na wasanii wenzake muda mfupi baada ya kutua.
Bi. Mwenda akiwa amembeba Matumaini mgongoni.
Matumaini (kulia) akiwa na Bi. Mwenda (wa pili kushoto) na anayefuata
(kushoto) ni msanii mwenzake Kiwewe wakisubiri gari la kumpeleka
hospitali.
Askari wakiwaelekeza wasanii kukaa upande mmoja ili apate hewa.
Matumaini akiwa amebebwa mgongoni na msanii mwenzake, Mariam Athuman ‘Kalunde’ akimpeleka kwenye gari.
Mama mkubwa wa Matumaini, Bi. Elizabeth (kushoto) na Matumaini
(katikati) wakiwa ndani ya gari tayari kuelekea hospitali ya Amana.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba
akizungumza na wasanii maeneo ya Amana wakati Matumaini akiwa kwa
daktari.
-----------
MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini
Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya
kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar
akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.
credit: Global