Warembo watatu wanaonekana kwenye video ya ngoma ya Tyga’s “Make it Nsty” wanadai ‘chuchu’ zao zimeonekana bila ruhusa yao.
Alissa
Rae Ross, Azia Davis, na Elizabeth Velasquez wamefungua mashtaka kwa
kudai kuwa walipofanya usaili kwaajili ya video hiyo kulikuwa na
kipengele kisemacho
“There will be NO ndity involved in the video, and all the girls will be tastefully shot.”
Kwa
mujibu wa madai yao Velasquez, Davis na Ross waliombwa wakati wa
kushoot video hiyo July 2, kutokea wakiwa vifua wazi katika baadhi ya
scenes lakini walihakikishiwa kuwa ‘chuchu’ zao zingefunikwa ama
kufanyiwa editing.
Katika mkataba wao wasichana hao wanadai kuambiwa kuwa “drty” version ya video hiyo isingetoka lakini ikatoka.
Wasichana hao wanashtaki kwa kukiuka mkataba, kuingiliwa usiri wao na madai mengine.