Mahabusu
mmoja ambaye hakufahamika mara moja mkazi wa jijini Arusha, ametoroka
chini ya ulinzi mkali wa polisi mahakamani hapo na kutokomea
kusikojulikana baada ya kufanikiwa kumnyang’anya silaha aina ya SMG
mmoja wa askari
polisi aliyekuwa akiwalinda wakati akitolewa kwenye
chumba cha mahabusu na kupandishwa kalandinga la polisi kurudishwa
gerezani .
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,limetokea majira ya saa 7.30 mchana
jana katika mahakama kuu jijini Arusha ambapo tukio hilo lilizua hofu
kubwa mahakamani hapo baada ya kuwalazimu baadhi ya watumishi wa
mahakama hiyo kujifungia ndani ya vyumba vya mahakama wakihofia mahabusu
huyo kuwafyatulia risasi.
Taarifa
zimedai kwamba mahabusu huyo alikuwa wa kwanza kutoka kwenye chumba cha
mahabusu na alipomkaribia askari huyo ambaye pia hajafahamika ghafla
alivaa na kumpora silaha hiyo inayodaiwa kuwa na risasi 30 na kuruka
uzio mrefu wa mahakama hiyo.
Mashuhuda
walisema kuwa mahabusu huyo wa jinsia ya kiume alitokomea na silaha
hiyo kwenye mto sanawari uliopo pembezoni mwa mahakama hiyo, hata hivyo
baadae aliitelekeza silaha hiyo na polisi walifanikiwa kuipata .
‘’unajua
tukio hilo limewashtua watu sana hawawatumishi wa mahakama walijifungia
ndani wakihofia usalama wao hata hawa watu wanaokaahapa kusikiliza kesi
za ndugu zao wote walitawanyika ‘’alisema shuhuda huyo n akuongeza kuwa
‘’si
jambo la kawaida kutokea ila kuna uzembe Fulani umefanywa na polisi
kwani haiwezekeni askari aporwe silaha tena SMG akiwa ameishikilia ,hii
ni hatari sana ‘’
Baada
ya tukio hilo polisi walianza kuhaha kumsaka mahabusu hiyo na kwamba
wakati wakipita eneo alilokimbilia walifanikiwa kuikuta bunduki hiyo
ikiwa imetelekeza kwenye mawe ene la mtoni.
Hata hivyo haikufahamika mara moja mahabusu huyo alikuwa akikabiliwa na makosa gani mahakamani hapo .
Kamanda
wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabasi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kwamba polisi inafanya uchunguzi wa tukio hilo
huku wakifanya msako mkali wa mahabusu hiyo.