17 October 2012

Angalia PICHA WATUHUMIWA wa KUCHOMA MAKANISA MBAGALA WAKIWA MAHAKAMANI


Watuhumiwa
wa vurugu za Mbagala wiki iliyopita, wakiwa chini ya ulinzi wa polisi,
walipofikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa
mara ya kwanza jana. Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa
mashtaka mbalimbali kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa
kuchomwa moto wiki iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa
kuwa waislamu, kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu.
Dhamana ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30.




Baadhi
ya watuhumiwa wa vurugu zilizotokea Mbagala jijini Dar es Salaam wiki
iliyoipita, wakiwa ndani ya gari la polisi walipofikishwa mahakama ya
hakimu Mkazi Kisutu jijini Oktoba 16, 2012 kwa mara ya kwanza.
Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka mbalimbali
kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto wiki
iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waislamu,
kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. Dhamana ya
watu hao itaamuliwa Oktoba 30.



Akina
mama wanaotuhumiwa kuhusika na vurugu zilizotokea  huko Mbagala,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, wakishuka kutoka
ndani ya gari la polisi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam jana. Akina mama hao ni miongoni mwa watuhumiwa 29
waliofikishwa kwenye mahakama hiyo kujibu mashtaka ya kuhusika na vurugu
za kuvamia makanisa, kuchoma, kuharibu mali na kuiba.



Polisi
aliyejihami kwa bunduki na radio ya mawasiliano, akishika doria kwenye
lango la kuingilia chumba cha mahakama ambako watu 29 walifikishwa
mahakamani hapo Jumanne Oktoba 16, 2012, wakikabiliwa na mashtaka kadhaa
ya kuvamia makanisa, kuharibu,  kuiba na kuchoma mali za makanisa hayo
wiki iliyopita huko Mbagala jijini Dar es Salaam. Wote wamerejeshwa
mahabusu hadi Oktoba 30 ambapo mahakimu waliokuwa wakisikiliza kesi
hiyo, wameahidi kutoa uamuzi juu ya hatma ya dhamana. 

Source:K-VIS BLOG

Comments system

Disqus Shortname