MBUNGE
wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joshua Nassari, ameshikilia
msimamo wa kupiga marufuku Mwenge wa Uhuru kufika jimboni kwake na
kuwataka wananchi kuupuuza akidai hauna tija kwa
maendeleo yao.
maendeleo yao.
Aliwataka
wananchi jimboni humo wakae mkao wa kula kwani jitihada za kuyatwaa
mashamba makubwa yanayomilikiwa na wageni, zinaendelea hivyo wawe
wavumilivu.
Bw.
Nassari aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa
Operesheni Sangara uliofanyika kwenye Kata ya Usa River, wilayani humo.
Aliwaataka
wananchi kuupuuza mwenge huo, kutoshiriki kuchangia mchango wowote na
kusisitiza kama mtu yeyote atabughudhiwa kutokana na ujio wa mwenge
amualifu.
“Sioni
sababu ya Mwenge wa Uhuru kukimbizwa maeneo mbalimbali nchini kwani
badala ya kuhamasisha maendeleo, umegeuka sehemu ya ufujaji wa fedha za
wananchi.
“Hali
hii inachangia umaskini wa Taifa na kuhamasiha maovu katika maeneo
yote ambayo mwengu huu unalala, nasema hivi, Mwenge wa Uhuru marufuku
kufika jimboni kwangu.
“Mtu
yeyote ambaye ataombwa mchango kwa ajili ya mwenge muiteni mwizi na
mimi nitakuwa wa kwanza kuuzima baada ya kufika jimboni kwangu,” alisema
Bw. Nassari.
Aliwataka
wananchi hao kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali
itikadi zao kisiasa na kuihadharisha Halmashauri ya Meru kuzingatia
maadili ya utendaji kazi na kuacha kuwabughudhi wananchi kwa
kuwachukulia bidhaa zao hasa wanapokusanya ushuru sokoni kupitia wakala
wao.
Akizungumzia suala la uvamizi wa mashamba, Bw. Nassari
aliwataka
wananchi kuwa wapole kwani anaandaa mkakati wa kuhakikisha ndani ya
miaka mitatu, wamiliki wa mashamba hayo wanakimbia wenyewe ili wananchi
waweze kujitwalia ardhi yao.
Katika
hatua nyingine, Bw. Nassari alisema fedha zilizotengwa na halmashauri
kwa maendeleo Kata ya Usa River, kuanzia Julai mosi mwaka huu hadi June
mwaka 2013, ni sh. milioni 54.3 ambazo zitatumika kuboresha
miundombinu na huduma ya maji safi.
Alisema
ukarabati wa barabara kutoka Usa River hadi Magadilishu umetengewa sh.
milioni nane na barabara za mji mdogo katika kata hiyo zenye urefu wa
kilometa tano, zitagharimu sh. milioni 75.
Katika
mkutano huo, wafuasi 15 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Tanzania
Labour Party (TLP) walitangaza kuvihama vyao vyao na kujiunga CHADEMA.
CHANZO MAJIRA
No comments:
Post a Comment