SAKATA la usajili wa beki Kelvin Yondani, limechuka sura mpya zaidi,
ambapo sasa uongozi wa Simba umepanga kujitoa katika Ligi Kuu Bara.
Hatua hiyo ya Simba inakuja kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
kupitia kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji,
kumuidhinisha beki huyo kuichezea Yanga kwa madai kuwa
, kwa mujibu wa kanuni ya 44 kifungu kidogo cha tatu, Yanga ilifuata taratibu za kumsajili.
, kwa mujibu wa kanuni ya 44 kifungu kidogo cha tatu, Yanga ilifuata taratibu za kumsajili.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zakaria Hans Pop muda mchacha baada ya maamuzi hayo, amesema
wamelazimika kuchukua uamuzi huo wa kutaka kuiondoa timu hiyo katika
ligi, kufuatia kutoridhishwa na jinsi suala la rufaa yao ya kupinga
Yondani kuitumikia Yanga, lililovyoshughulikiwa.
Hans Pop amesema wamesikitishwa na hatua ya mwenyekiti wa kamati hiyo ya
TFF, Alex Mgongolwa kutaka mfumo wa kupiga kura, ndiyo utumike, badala
ya kufuata vifungu vya sheria.
“Kwanza alifanya uamuzi huo (wa kupiga kura) akijua wazi kuwa katika
kamati yake kuna wajumbe wengi wenye maslahi na Yanga ambao ni Lloyd
Nchunga na Iman Madega ambao waliwahi kuwa viongozi wa juu Yanga pamoja
na yeye mwenyewe (Mgongolwa) ambaye ana mapenzi na Yanga.
“Kuna wanachama wetu leo (jana) au kesho (leo) wataenda mahakamani kuishtaki TFF,” alisema Hans Pop na akiongeza:
“Baada ya ya baadhi ya wanachama hao kufungua kesi, sisi pia kama
uongozi tunakutana kesho (leo), baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya
Azam. Tunataka kuandaa mkutano mkuu wa dharura kuwaomba wanachama wetu
watupe idhini ya kujitoa ligi kuu.
“Likikamilika hilo na lile la kufungua kesi, tunaamini TFF watatufungia
kufuatia kupeleka masuala ya michezo katika mahakama za kiraia na baada
ya hapo na wao (TFF) watafungiwa na Fifa na hapo ndiyo lengo letu
litakamilika la kutaka mpira usichezeke hapa nchini.”
No comments:
Post a Comment