MODRIC AOMBA RADHI KWA KUKOMA KUSAFIRI NA TIMU.
KIUNGO wa kimataifa wa
Croatia na klabu ya Tottenham Hotspurs Luka Modric ameomba radhi kwa
mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy kwa kufanya mgomo na kushindwa
kusafiri na wenzake katika ziara Marekani. Kiungo huyo alipita katika
makao makuu wa klabu hiyo kumuomba radhi Levy kutokana na tukio hilo
kabla ya kupanda ndege kwenda kujiunga na wenzake waliopo katika ziara
nchini Marekani kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu nchini
Uingereza. Modric ambaye ana umri wa miaka 26 alitegemea mgomo aliofanya
wa kukataa kusafiri na timu katika uwanja wa ndege wa Heathrow juzi
itasaidia kutoa msukumo wa kukamilika kwa mchakato wa kumuuza katika
timu ya Real Madrid. Lakini mbinu hiyo ilionekana kumkera Levy ambaye
alitaka kumtoza faini ya paundi 15,000 katika kila siku ambayo atakuwa
akiendelea na mgomo huo. Naye meneja wa Spurs Andre Villas-Boas
ameonyesha kukerwa na kitendo hicho na kusema kuwa hakutegemea kufanywa
na mchezaji mwenye hadhi kama ya Modric lakini anategemea suala hilo
limalizika haraka ili waweze kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa
ligi.
No comments:
Post a Comment