18 April 2012

Mbunge wa Temeke Abass Mtevu apata ajali AKIWA NJIANI KUELEKEA DAR ES SALAAM

Mbunge wa Temeke  
Abass Mtevu na dereva 
wake ambaye jina lake
 hakutajwa, wamenusurika 
kifo baada ya kupata

 ajali ya gari  wakiwa 
njiani kuja Dar es Salaam.


Akitoa taarifa bungeni 

mchana huu, 
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai 
amesema baada ya ajali iliyosababishia
 majeraha kadhaa mwilini, Mtemvu na
 dereva wake wametibiwa katika
 hospitali ya Morogoro na 
kuruhusiwa kuja Dar.


"Wamenusurika ingawa wamepata

 majera kadhaa mwilini, na hivi 
ninavyozungumza wapo njiani
 kwenda Dar es Salaam" alisema 
Ndugai kuwaambia wabunge.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname