30 June 2015

MAMA WEMA SEPETU AMPIGA VIBAO ASKARI HADHARANI!

Mama mzaa chema wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu.
Haya ni madai mazito! Mama mzaa chema wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu anadaiwa kumzaba vibao askari wa kampuni binafsi.Kwa mujibu wa shuhuda huyo, tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi lilijiri kwenye Bandari ya Dar es Salaam, majira ya mchana Ijumaa iliyopita.Kabla ya kushusha stori kamili, Ijumaa Wikienda lilimhoji shuhuda huyo kama anamjua vizuri mama Wema ambapo alithibitisha kuwa ni yeye huku akisapotiwa na wenzake waliokuwa wakisikika kwenye simu
“Nani asiyemjua mama wa staa mkubwa kama Wema? Tena kafuatana na Wema mwenyewe. Kila mtu hapa anamjua ngoja tujaribu kupata picha zake nzuri,” alisema shuhuda huyo kwa kujiamini.
Shuhuda huyo alidai kwamba chanzo cha yote, mama Wema alidaiwa kutumia mlango usio sahihi na alipofuatwa kuelekezwa ndipo likaibuka timbwili zito. 
 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname