katika pitapita zangu kwenye
mitandao ya kijamii nimekutana na picha moja safi ya mshambuliaji hatari
wa Azam fc, Muivory Coast, Kipre Tchetche akiwa amevalia jezi ya
mabingwa wa soka Tanzania bara, Dar Young Africans.
Tchetche ameonekana akipiga stori na Mrembo aliyeketi pembeni yake, bila shaka wanamwambia jambo nyeti! hahahahah!
Stori ya ndani inasema kwamba
kocha aliyerejea Azam fc, Stewart Hall bado anahitaji huduma ya
Tchetche, lakini moja ya mabosi wa Azam hawamtaki mchezaji huyo.
Msimu uliopita nyota huyo
anayecheza nafasi zote za mbele alikosa mechi nyingi kwasababu za
majeruhi, lakini kuna wakati alifungiwa na klabu yake kwasababu ya utovu
wa nidhamu.
Hata hivyo Tchetche alishuka kiwango tofauti na misimu miwili ya nyuma, kitendo kilichowaudhi matajairi wa Azam fc.
Je, kuvaa jezi ya Yanga kunaashiria nini wakati huu wanajangwani wanajipanga kuanza usajili wa kimataifa?
No comments:
Post a Comment