23 December 2014

DEREVA AJISHINDA MTOKO WA MBUGANI KATIKA PROMOSHENI YA TUTOKE NA SERENGETI



SERENGETI BREWERIES LTD

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DEREVA AJISHINDA MTOKO WA MBUGANI KATIKA PROMOSHENI YA TUTOKE NA SERENGETI
Tarehe 23/12/2014, Dar es Salaam,
Bw. Deogratias Peter Masenga mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni dereva wa malori makubwa na mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro atasherekea sikukuu ya krismasi kwa staili ya aina yake baada ya kuibuka mshindi wa safari inayogharamiwa na SBL kupitia kampeni yake inayojulikana kama ‘Tutoke na Serengeti’.

Deo alitangazwa mshindi katika safari ya “MTOKO WA MBUGANI” kupitia droo ya kawaida ya kila wiki iliyofanywa katika ofisi za Serengeti katika mazingira ya uwazi na kushuhudiwa na vyombo vya habari mbalimbali, Price Water Coopers (PWC) na maafisa kutoka Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Moshi mjini kwa shughuli zake za kikazi, Bw, Deo ambaye alijawa na bashasha mara baada ya kupata taarifa hizo alisema “Hii ni mara yake ya kwanza kushinda kitu cha namna hii. Nina furaha sana kuibuka mshindi, hakika naumaliza mwaka kwa staili ya aina yake nawashukuru sana Serengeti”. 

Deo ambaye alimchagua kaka yake kama mtu wa kwenda naye kwenye safari hiyo, aliwashauri watu wengine wasikate tamaa na kujaribu kushiriki mara kwa mara katika promosheni hii .
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Bia ya Serengeti, Bw. Elihuruma Ngowi alisema …”Kampuni ya Serengeti itatumia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 10 kwa ajili ya safari ya mshindi na anaruhusiwa kwenda na mwenza au mtu yeyote atakaye mpendekeza kwenye mtoko huu wa siku mbili katika mbuga ya wanyama ya Serengeti…. Kiasi kilichotajwa kitawawezesha kupata fedha za kujikimu, malazi, usafiri na mambo mengine,” aliongeza Elihuruma

Bw. Elihuruma alisisitiza kwamba promosheni hiyo bado inaendelea na milango ipo wazi kwa wateja wote na kuwaomba waendelee kujitokeza kushiriki “Bado kuna washindi watatu watakaoshinda safari hii ya Serengeti, kwa hiyo nachukua fursa hii kuwatia moyo wateja wote wa Serengeti kuendelea kushiriki kwenye promosheni hii ya aina yake”.

Ili kuweza kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kununua bia ya Serengeti Premium Lager na kuangalia ndani ya vizibo na kuna namba ambazo wanapaswa kuzituma kupitia ujumbe wa simu za mkononi (sms) kwenda 15317 na moja kwa moja wataingia kwenye droo na kuweza kushida zawadi kama vile Limo Bajaj, Pesa Taslimu, Punguzo la shilingi 300 kwenye bia na bia za bure na unavyozidi kutuma namba hizo kutoka kwenye vizibo ndipo unapojihakikishia nafasi ya kushida.

Kwa Taarifa zaidi Tembelea.
Tembelea kurusa za facebook na twitter za Serengeti Premium Lager

ABOUT SERENGETI BREWERIES LIMITED
Serengeti Breweries Limited engages in the brewing, manufacturing, marketing and selling drinks made of malt, hops and barley and sorghum in Tanzania.
 Headquartered in Dar es Salaam, SBL brands include:- Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick and Guinness®.
 SBL is also the sole distributor of several international renowned spirits including Smirnoff Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and Gilbeys Gin®.
 Serengeti Breweries Limited is a subsidiary of East African Breweries Limited/ DIAGEO PLC.

Kaimu meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, Elihuruma Ngowi, akiongea kwa simu ya mkononi na mshindi wa pili wa shindano la “Tutoke na Serengeti” wakati wa kuchezesha droo katika shindano la Tutoke na Serengeti ambapo, Bw. Deogratius Peter Masenga kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro ameibuka mshindi, kulia ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Mrisho Millao. Hafla ya kuchezesha shindano hilo ilifanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam.




Kaimu meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, Elihuruma Ngowi,(katikati) akiongea kwa simu ya mkononi na mshindi wa pili wa shindano la “Tutoke na Serengeti” wakati wa kuchezesha shindano hilo ambapo , Bw.Deogratius Peter, toka Rombo Kilimanjaro ameibuka mshindi, (kulia) ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Mrisho Millao na kushoto ni Meneja mwendeshaji wa kanda  Serengeti , Malalia Mmassy. Hafla ya kuchezesha shindano hilo ilifanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname