Kijana Simon Manase (22) aliyecharangwa mapanga baada ya kufumaniwa na mke wa mtu vichakani.
MH! ‘Haga gangi’ (haya mengine)! Simon Manase (22) ambaye ni dereva wa bodaboda, mkazi wa Kijiji cha Nguyami, wilayani Gairo mkoani hapa amecharangwa mapanga mwilini na kukatwa mkono wa kulia na mtu aliyetajwa kwa jina la Frank akidai kumfumania na mkewe vichakani.
Ishu hiyo inadaiwa kujiri usiku mnene wa Oktoba 31, mwaka huu kwenye Kijiji cha Nembo mpakani mwa Gairo na Kilosa katika muziki wa mitaani maarufu kwa jina la ‘kigodoro’.Mwandishi wetu alipiga gia hadi kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kuzungumza na mashuhuda, viongozi wa kata, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Berega na Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila.
“Siku ya tukio tulikuwa kwenye shereha ya mwenzetu, mwanae amevunja ungo hivyo nyumbani kwake aliweka muziki wa kigodoro, cha ajabu ilipofika saa sita usiku DJ wa muziki, Alex Munga alitutangazia kwamba kuna watu wanapigana mapanga baada ya kufumaniana kwenye kichaka.
Simon Manase akiuguza majeraha katika Hospitalini ya Berega mkoani Morogoro.SOMA ZAIDI>>>


No comments:
Post a Comment