Mwigizaji wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’.
AMA kweli
fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye,
Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka, ungana na .
Habari
za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala
anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
Kwa mujibu wa chanzo makini
kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo
ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa
akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha
wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga
kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY
Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa
analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya
Sinza-Madukani jijini Dar.
No comments:
Post a Comment