NI maajabu ya dunia! Mke wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT ‘Bonde la Baraka’ lililopo Kata ya Kerege Manofu, Bagamoyo mkoani Pwani, Boniface Onesmo Mahera (38) (pichani), Bentha Seth (27) baada ya kubeba mimba kwa miezi tisa hatimaye amejifungua hirizi, gazeti la kijamii, Uwazi lina mkasa wote.
Akizungumza na waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mchungaji huyo alisema mbali na mkewe kujifungua hirizi, pia alitoa mawe mawili, mkaa usiotumika na kitambaa chekundu chenye ukumbwa wa ‘hendkachifu’.NI MIMBA YA TATU KUTOKA KIMAAJABU
Akisimulia mkasa huo, mchungaji huyo alisema kuwa, awali mkewe alikuwa akipata ujauzito lakini ukifikisha miezi mitatu hutoka.“Tangu mwaka 2009 zimeshatoka mimba tatu kimaajabu.
Alikuwa akishika ujauzito, ukifikisha miezi mitatu unatoka akienda kujisaidia, hali ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba tulikuwa tunafanya maombi kila mara na wakati huo wote mimi nilikuwa bado sijasimikwa kuwa mchungaji,” alisema mchungaji huyo.
No comments:
Post a Comment