Dully
amedai kuwa Alikiba na Diamond wanatakiwa wafanye kazi waweke tofauti
zao pembeni na waingize hela. “Hivi we unadhani itoke nyimbo ya Alikiba
na Diamond si itakuwa hatari sana! Maana hiyo ngoma itakuwa gumzo na
pia wata watawafurahisha mashabiki wao. Huo ndo ushauri kwa wadogo
zangu,” amesema Dully
Katika
hatua nyingine Dully amesema sababu za kutofanya vizuri kwa nyimbo zake
za sasa. “Unajua nyimbo yangu kama ile ya “Joka” haikufanya
vizuri kwakuwa watu walihisi kama nimemdiss mtu ndo maana haikufanya
vizuri. Kwa wimbo wa “Binti Spesho” nao ulishindwa kufanya vizuri hasa
ilivyofungiwa video yake lakini sasa wimbo wa ,’Togola’ unafanya vizuri
nadhani pia umetoka kipindi kizuri na pia video yake ipo tayari inatoka
muda wowote kuanzia sasa.
Kuhusu kazi yake kama mtayarishaji wa muziki, Dully amedai kuwa anazidi kuifurahia.
“Tokea
nimekuwa producer naenjoy sana maana napenda sana kazi ya kuwa producer
sasa hivi kuliko hata kuimba. Na pia sasa nimeshafanya kazi kadhaa za
wasanii wakubwa zinakuja
kama ya Chidi Benz vile imeshatoka na kuna zingine zinakuja. Unajua
sasa hivi studio yangu ina vyombo vipya vya kisasa na pia ntakuwa
narekodi live yaani napiga vyombo vyote
No comments:
Post a Comment