MSANII wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni alionesha
jeuri ya magari baada ya kutinga nayo mawili kwa nyakati tofauti kwenye
kumbukumbu ya miaka miwili ya marehemu Steven Kanumba.
Awali kwenye ibada ya kumuombea marehemu, Kajala alifika kwenye
kanisa moja lililopo
Kimara Temboni akiwa ‘anadraivu’ gari aina ya
Toyota Harrier nyeusi na kuzua gumzo eneo hilo
Baadaye msafara ulipohamia Makaburi ya Kinondoni alipozikwa Kanumba,
alitinga na gari lingine aina ya Toyota Brevis lile ambalo ilidaiwa kuwa
alinunuliwa na yule kigogo wa shosti wake, Wema Sepetu anayejulikana
kwa jina la CK.
Jeuri hiyo iliwafanya wengi kubaki na vingi viulizo na Ijumaa
lilipojaribu kumdadisi hakutoa ushirikiano na hata alipopigiwa simu
baadaye hakupatikana hewani
No comments:
Post a Comment