Je, Unadhani ukiulizwa hilo swali utajibu nini kwa upande wako?
Tafiti
mbalimbali za mahusiono ya kimaapenzi zinaeleza kuwa watu wengi hujibu
mara tatu na kuendelea lakini bado wanadai kuwa hawatosheki na viwango
hivyo na kuliacha swali kubaki kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki
ili watosheke?
Jibu la swali hili linapatikana baada ya
kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha kutosheka hasa nini?
Katika hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na wala si mwilini,
hii ina maana kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri
unavyodai ni njia ya kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya
mwili haitoki mwilini bali kwenye akili ya mtu.
Kwa msingi huo
mtu akitaka kutosheka na penzi la mpenzi wake, ni lazima kwanza
aitosheleze akili yake na kile anachopata, zoezi ambalo atalifikia kwa
kutathimini uwezo wake wa kufanya mapenzi na wa mpenzi wake. Wengi kati
ya watu wanaodai hawatosheki kimapenzi ni wale wanaoziachia akili zao
zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya
yao ya kukutana kimwili.
Nikijibu swali la ni mara ngapi wapenzi
wakutane kimwili ili watosheke nitasema hivi: KUTOSHEKA HAKUNA IDADI,
bali ni kwa kila mmoja kulidhika na mwenza wake kutoka ndani ya akili
yake. Kama hapa sikueleweka vizuri katika jibu hilo, maana yangu hasa ni
kwamba kutosheka ni namna mtu mwenyewe anavyoyaendesha mawazo yake.
Ukiyaendesha
mawazo yako kufanya mapenzi mara kwa mara, hutatosheka hata ukipewa
kila saa, kwa sababu fikra zako unazijenga zaidi ya unachopata.
Uchunguzi unaonesha kuwa watu ambao akili zao zimejaa mawazo ya ngono,
hawawezi kulala bila kufanya mapenzi, lakini watu hao hao, ukiwapa
matatizo yatakayochukua sehemu kubwa ya mawazo yao kwa mfano, kuwafunga
jela, kuwafukuza kazi, kupata msiba, utashangaa wanaweza kukata wiki
bila kusumbuliwa na tamaa ya ngono.
Hii ina maana kwamba
unavyowaza ndivyo unavyotenda. Kitaalamu kinachofanya mapenzi ni mawazo,
ndiyo maana wapo wanaojichua wenyewe kwa kutumia mawazo yao na kupata
raha. Kila mmoja akijenga heshima juu ya fikra zake na kujali hisia
zaidi tutakuwa na watu wengi wanaofurahia tendo la ndoa bila kujali
wanalipata mara ngapi kwa wiki.
Uchunguzi unabaini umebaini kuwa
watu wengi hasa wapenzi wa siku nyingi na wanandoa, wanafanya mapenzi
kwa sababu tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja, lakini si kwa kuheshimu
fikra na hisia zao, jambo ambalo husababisha ladha ya mapenzi kuwa ya
asilimia ndogo, ukilinganisha na mahitaji halisi ya mawazo yao.
Upo
ushahidi wa kutosha kwa wanandoa wengi kupata msisimko mdogo wanapokuwa
na waume/wake zao katika tendo la ndoa tofauti na wanapopata wasaa wa
kusaliti ndoa kwa hawara zao.
Watu wa aina hii wasiseme kuwa
hawatosheki na tendo la ndoa kwa sababu wanakutana na wapenzi wao mara
chache zaidi, bali wanakutana katika mhemko wa chini usioweza kulifanya
tendo hilo kuwa na raha ya kutosha.
Labda msomaji wangu
utaniuliza, tatizo la kupata msisimko mdogo kwa mtu unayemzoea
linachangiwa na nini? Jibu litakuwa ni MAWAZO ya mtu mwenyewe.
Ukichunguza utagundua kuwa, wapenzi wengi hasa wazoefu huwa hawapeani
nafasi katika mawazo, kamawanavyotoa nafasi kwa wapenzi wa pembeni, hili
ndilo tatizo linalopunguza msisimko wa kimapenzi na kuondoa hali ya
kutosheka na penzi. Kama mtu anataka mpenzi wake amtosheleze, basi hana
budi kumkuzia mwenza wake hisia kiasi cha kumtamani. Niulize swali,
hivi ni mara ngapi wewe unayesema hutosheki na penzi ulishakaa peke yako
ukamvutia taswira mpenzi wao kabla hajarudi nyumbani kiasi cha kupata
msisimko wa kutana naye kimwili?
Wengi wetu hatufanyi hivyo,
hatuna vitu vinavyotuvutia kwa wake/waume zetu, jambo ambalo hutufanya
tukikutana nao kimwili kwa kutimiza desturi tu na kubaki na kiu zetu za
penzi. Lakini ukweli unabaki kuwa wapenzi wakikutana kipindi cha
msisimko mkubwa na kupeana mahaba kwa usahihi hata ikiwa ni mara moja
kwa wiki watatosheka.
Jambo kubwa la kuzingatia hapa ni kwamba
wakati mwingine msisimko huo huwa hauwatokei wapenzi kwa wakati mmoja,
hivyo ni jukumu lao kushirikiana pindi mmoja anapokuwa katika hali hiyo.

No comments:
Post a Comment