18 August 2014

UKOSEFU WA FEDHA ZA KUJIKIMU WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAZUA BALAA WAGEUKA KUWA OMBAOMBA.

WAZIRI  wa sheria na katiba wa serikali ya wanafunzi kutoka chuo cha usimamizi wa fedha IFM kilichopo jijini Dar es salaam Kasanzu Luganga ambaye yuko Shinyanga kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa vitendo ofisi ya bima ya afya (NHIF),akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga ,ambapo alisema tangu waanze mazoezi kwa vitendo miezi miwili imepita hakuna fedha iliyotumwa na serikali kwa ajili ya kujikimu wakati wa (Field) hali ambayo imesababisha waishi katika mazingira magumu kwa kuomba omba fedha kwa ndugu,jamaa na marafiki ili waweze kujikimu kimaisha.     Alisema kuchelewa kwa fedha za kujikimu wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wako katika mazoezi ya vitendo mkoani Shinyanga,kumesababisha baadhi yao kugeuka kuwa ombaomba  kutokana na kukosa fedha za kulipia kodi za nyumba walizopanga na huduma zingine muhimu ikiwa ni pamoja na kununu  chakula na matibabu na ameitaka serikali kutoa fedha hizo sh 620,000 kwa mwezi ili kuwaondolea kero.

  

Gabriel Ndogani mwanafunzi wa elimu ya juu mwaka wa pili chuo cha IFM ambaye anafanya mazoezi kwa vitendo ofisi ya NSSF Shinyanga,alisema inashangaza kuona serikali inachelewa kutoa fedha hizo wakati zilipitishwa kwenye bajeti sh 6.6 bilion zimekwenda wapi au zimetumika kinyume cha walengwa waliokusudiwa na kutaka hata wabunge wa bunge maalumu la katiba nao serikali isiwalipe iwakope  kama fedha hakuna lakini mbona wanasaini kila siku iwaje sisi wanafunzi tusilipwe fedha za field.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname