Mwanamziki mashuhuri wa miondoko ya Hip-Hop hapa nchini,
Roma Mkatoliki ametangaza rasmi kuachia ngoma zake mpya usiku wa Serengeti
Fiesta-Tanga, katika uwanja wa Mkwakwani jumamosi hiii.
Mwanamuziki huyo ambaye ni Mzaliwa wa Tanga na kipenzi cha
wengi Jijiji hapo amesema kwamba, ngoma hizo mpya zitasindikizwa na vibao kama
vile Mr. President, Pastor, Mathematics, 2013, KKK pamoja na ngoma mbalimbali
alizoshirikishwa na wasanii mbalimbali nje na ndani ya nchi.
alizoshirikishwa na wasanii mbalimbali nje na ndani ya nchi.
Kauli mbiu ya Serengeti Fiesta mwaka huu ni “Sambaza
upendo,”
Roma ambaye kwa sasa ni kati ya wanamuziki wakubwa hapa
nchini, amekuwa akishiriki Serengeti Fiesta tangu mwaka 2007.
“Serengeti Fiesta imenikuza kumuziki…nimeanza kupanda katika
majukwaa ya Serengeti fiesta miaka saba iliyopita na katika kipindi chote hicho
nimekuwa nikipata ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa mashabiki zangu na
nnamshukuru Mungu kwamba sijawahi waangusha mashabiki zangu,” alisema Roma.
Roma ameishukuru Serengeti Fiesta kwa kuwakutanisha wasanii
mbalimbali kutoka pande zote hapa nchini. “Kupitia Serengeti fiesta, imekuwa
rahisi sana kwa wasanii kubadirishana mawazo…kukutana na mashabiki zetu na vile
vile kipata fursa mbalimbali ambazo si rahisi kuzipata tukiwa mtaani.”
Roma amewaasa wasanii na wadau wa muziki kutumia fursa
vizuri fursa zinazoambatana na serengeti fiesta ili kujinufaisha kimuziki na
katika maisha yao ya kawaida.
Wasanii wengine watakao lipamba jukwaa la Serengeti Fiesta
Tanga ni pamoja Recho, Chege and temba, Alikiba, Ney wa mitego, Stamina, Jux,
Linah, Vanessa mdee, Mr Blue, Mkubwa na wanae, Ommy
Dimpoz, Barnaba, Young Killer na Madee.
Waandaaji wa tamasha hili wamewahakikishia Wanatanga usalama
wa hali ya juu na kusema kwamba serikali ya Jiji la Mwanza iko makini na itatoa
ulinzi tangu mwanzo wa tamasha mpaka mwisho.
Baada ya Tanga, burudani hili la nguvu litashuka katika
mikoa mbalimbali kama Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Moshi, Arusha,
Mtwara na Dar es salaam na hatimaye
jijini Dar es Salaam ifikapo oktoba 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment