Kama ulimuona Sylvester Stallone kwenye Expandables, bila shaka
uliona umri wake ulivyo mkubwa huku akiendelea kutisha kama bado ni
kijana mdogo. Sasa utamshangaa zaidi mama yake mzazi, Jackie mwenye
miaka 92 anaeamini umri sio kikwazo.
Bibi huyo ameendelea kufanya mazoezi ya viungo licha ya kuwa na umri
mkubwa na hata anapokuwa gym hubeba hadi vyuma vyenye uzito huku
akisaidiwa kwa ukaribu na watu.
Bibi Jackie bado anavaa Mini-Skirt, na kupaka make up kama wanavyofanya wasichana warembo wenye umri mdogo.
“Hollywood wanahofia umri, lakini nadhani wazee ndio wanakuja.
Nadhani umri wa mwanamke wa kati unarudi. Wote tungependa kufika kule,
kufika kule kama mimi. Sio kwenye kiti cha kukusaidia kutembea, wala
kuwa kwenye kitu maalum cha kutunzwa.” Amesema mama Rambo.
No comments:
Post a Comment