Shostito wa Aunt Ezekiel, Nice Chande.
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na shostito wake Nice Chande, juzikati walijikuta walitifuana kwa matusi makali ya nguoni nyumbani kwa rafiki yao Wema Sepetu ‘Madam’ anayeishi mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.Chanzo makini cha habari kilichokuwa nyumbani kwa Wema, kililidokeza gazeti hili kuwa waigizaji hao wakiwa na rafiki yao mwingine, walianza kutukanana kwa jambo ambalo halikuweza kubainika mara moja, huku Madam akijitahidi kuwasuluhisha bila mafanikio.
Wakiwa na dalili zote za kubugia kiburudisho cha kutosha kilichowafanya wasione vibaya kupaza sauti za matusi mbele za watu, marafiki hao walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuendelea kutukanana kana kwamba hawana akili nzuri.

No comments:
Post a Comment