Mama Wema Sepetu Aanza Kumkubali Diamond Platnumz, Wema Ajawa Na Furaha.
 |
| Wema na mama yake mzazi |
Baada ya Mariam Sepetu ambaye ni mama mzazi wa Wema Sepetu kutokumkubali
Diamond Platnumz kama mpenzi wa mwanae hatamaye mama Wema ameanza
kumkubali Diamond. Akizungumza na Globalpublishers Wema amesema kuwa kwa
muda mrefu alikuwa hana maelewano mazuri na mama yake sababu ya uchumba
wake na superstar huyo wa Bongofleva lakini kwasasa ameanza kumkubali
"Mama
nilikuwa nikimsihi sana juu ya uchumba wangu na Diamond lakini sasa
tumefikia hatua nzuri namshukuru Mungu amekubali, maana siku hizi
nikionana naye ananiuliza vipi mwenzako mzima, anaendeleaje, wakati
mwanzoni haikuwa hivyo" alisema Wema
No comments:
Post a Comment