Johanitha Robert Mulokozi amekaa kitandani kwa miaka mitatu kutokana na kuugua ugonjwa wa kupooza mwili mzima.
INASIKITISHA! Johanitha Robert Mulokozi (31) amekuwa kitandani kwa miaka mitatu kutokana na kuugua ugonjwa wa kupooza mwili mzima.Mama huyo mwenye mtoto mmoja amekuwa akisumbuka na ugonjwa huo uliomfanya akose raha licha ya kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumza na waandishi wetu nyumbani kwake Nyan’gandu, Kivule, Ilala jijini Dar es Salaam, mama wa mgonjwa huyo, Valentina Emmanuel (51) alisema kwa miaka mitatu anashindwa kupata usingizi kutokana na kumuuguza mwanaye huyo na kukosa uwezo wa kumsafirisha kwenda India kwa matibabu.
“Sikutegemea kama mwanangu angekuwa hivi kwani alikuwa akiishi vizuri na alikuwa akiendelea na maisha yake hasa baada ya kupata mtoto ambaye anamtegemea.SOMA ZAIDI>>
No comments:
Post a Comment