Studio ya Bob Junior imebadilika kutoka ‘Sharobaro Records’
na kuwa ‘Sharobaro Music’.
Bob Junior ameiambia Blog hii kuwa sababu za kubadilisha
jina hilo ni kutokana na kubadilika kwa muziki atakaokuwa akiutengeneza kama
mtayarishaji wa muziki na pia kutokana na kununua vifaa vipya.
“Ilikuwa ni mahesabu ya kwangu mimi na kampuni yangu,
tulikuwa tunataka kuibadilisha kuanzia muziki, sound kwasababu kuna vyombo
vipya ambavyo vimekuja kutoka Marekani na pia nilikuwa nimetengeneza sound mpya
siku nyingi,” amesema.
Mtayarishaji huyo wa muziki amedai kuwa uamuzi huo umekuja
ili kuwathibitishia watu kuwa anaweza kufanya muziki wa aina mbalimbali.CHANZO Kikwetu Blog
No comments:
Post a Comment