Dogo anaswa na mkoko? Huo mkoko mmemnasa nao wapi wakati hizo picha ni mimi nilizi post mwezi February Instagram?????
Picha ambazo zilipigwa Nyumbani lounge tena kutumia simu ya Gardner.
Jide, dogodogo gumzo mjini
Gumzo ni kitu kinachoongelewa sana na kilichoenea kila kona ,,,,,sasa hii habari ni gumzo wapi ambapo haisikiki, ......
Mngeandika tumeamua kumuanzishia Jide gumzo hili, ndio ningewaelewa.
Vitu vya kuzua.

Ni watu wengi tu wakija band wakipata nafasi wanaomba kupiga picha na mimi na wengine pia wanaomba kupiga picha na gari sababu wanaipenda.
Kama mtu yoyote anavyoweza kupiga picha na sanamu la kitu chochote anachokipenda. Hivi je! Wimbo wa JayDee mgumba, JayDee tasa umechuja? Umeisha chati?? Nashangaa na najiuliza tu

No comments:
Post a Comment