23 August 2014
DIAMOND THE PLATNUMZ ATANGAZA RASMI NDOA YAKE NA WEMA SEPETU
KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za mauzo
nchini ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi kipya
Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema
Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na
Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano.
Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo
maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo. “Ndoa
ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo
yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata
ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la
kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake. “Nataka kila
kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,”
aliongeza. “Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu
wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu
zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram
tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.” Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo
Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu
vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye
anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili
vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo
ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment