08 May 2014

MGONJWA ALIYELAZWA HOSPITALI KWA MIAKA 45

 
Lanjui aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu Januari Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, Mwanza kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.
SINGIDA. 
Usiombe yakupate. Abdi Lanjui (75), ametimiza mwaka wa 45 akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu mwaka 1971 baada ya kupata ajali ya lori. 
Lanjui aliyekuwa dereva wa taasisi aliyoiita “Mamlaka ya Pamba,” alipata ajali hiyo mkoani Mwanza baada ya lori alilokuwa akiendesha kuchomoka gurudumu la mbele na kupinduka. 
“Sababu ya mimi kugeuza wodi kuwa makazi yangu ya kudumu ni ajali iliyosababisha kupooza kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo. Kwa kuwa sinyanyuki kitandani, nimepata vidonda kuanzia makalioni hadi miguuni. Kwa sasa naishi maisha magumu mno,” alisema. Aomba msaada Kutokana na hali hiyo, ameiomba Serikali na jamii kwa jumla kumsaidia chakula kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia. Lanjui ambaye hawezi kunyanyuka kitandani, alisema kwa miaka mingi uongozi wa hospitali ya mkoa ulikuwa ukimhudumia kwa kumpa chakula lakini baadaye huduma hiyo ilisitishwa, hivyo kumfanya awe ombaomba na maisha yake kuwa ya mlo mmoja kwa siku. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname