
Meneja
wa zamani wa Manchester United David Moyes anachunguzwa na polisi
kufuatia mtafaruku katika baa moja nchini Uingereza. Maafisa wa polisi
waliitwa katika baa ya Emporium mjini Clitheroe siku ya Jumatano,
kufuatia taarifa kuwa mtu mwenye umri wa miaka 23 kushambuliwa. Polisi wa Lancashire
wamesema
mtu aliyepigwa hakuhitaji matibabu ya hospitali. Msemaji wa polisi
amesema maafisa wanajaribu kuchunguza nini hasa kilitokea. Moyes
aliachishwa kazi ya umeneja wa Manchester United miezi 10 baada ya
kupewa kazi hiyo, akitokea Everton.
No comments:
Post a Comment