Wanasayansi nchini Brazil wamegundua aina ya nyoka
vipofu wenye umbo kama uume wa binadamu.
Tuwie radhi kama picha hizi zitakuondolea hamu ya kula
lakini huu ni uumbaji wa Mungu.
Nyoka hawa wa ajabu aina ya ‘atretochoana eiselti’
walipatikana kwenye bwawa la kuzalisha umeme ambapo wakandarasi walikuwa wakifanya
ukarabati kwenye misitu ya Amazon.
Wana baiolojia waliwapata nyoka hawa wenye umbo la ajabu
sita wenye urefu wa mita moja chini ya mto Madeira huko Rondonia, Brazil.
Nyoka huyo anaweza akawa na muonekano usiopendeza lakini
huu ni ugunduzi unaovutia kwa wanayasansi wanaomini kuwa wanauhusiano na vyura.
Wanasayansi wamesema licha ya viumbe hao kuonekana kama nyoka lakini sio jamii ya reptilia.
Je wanasumu kama nyoka hawatuliowazoea?
ReplyDelete