11 April 2014

Taarifa kuhusu mchezaji wa zamani wa Arsenal kujiunga na vita ya jihad Syria


Bky67_lCAAAH5k7
Kiungo wa zamani wa Arsenal na Real Madrid anayekipiga katika klabu ya Lokomotiv Moscow Lassana Diarra amekanusha madai kwamba ni mfuasi wa vita ya kidini nchini Syria.Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Diarra (29) alijiunga na vita inayoendelea Syria baada ya kutolewa kwa video inayomuonyesha mtu akiwa kajifunika uso huku akijitambulisha kwamba ni Lassana Diarra.Hata hivyo kiungo huyu wa timu ya taifa ya Ufaransa ambae aliwahi pia kuitumikia Portsmouth na Chelsea, ametoa taarifa rasmi kupitia wakili wake na kusema hahusiki kabisa na hiyo video.“Hajawahi kukanyaga nchini Syria, ni ujinga na yeye sio mfuasi wa jihad, ni mwanasoka anayeichezea Lokomotiv Moscow,” amesema Mwanasheria wake.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname