23 February 2014

SHAMSA FORD WA BONGO MOVIE KAWEKWA 'NDANI' KIMYA KIMYA

WAKATI wadau wa filamu za Kibongo wakisubiri kwa hamu kushuhudia ndoa ya staa wao, Shamsa Ford imebainika kwamba msanii huyo ameshapigwa ndoa ya kimyakimya na mchumba wake wa muda mrefu ambaye pia ni mzazi mwenzake, Dickson ‘Dick’. Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wanadaiwa kufunga ndoa ya kimila nyumbani kwa mwanaume huyo, Tarime mkoani Mara wiki kadhaa zilizopita.
“Shamsa na Dick tayari wamefunga ndoa ya kimila kijijini kwa mwanaume Tarime ambapo walichinjiwa mbuzi na kufanyiwa mambo mbalimbali ya kimila lakini wenyewe wanafanya siri,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Shamsa ili kupata ukweli wa habari hizo na staa huyo alikiri kufunga ndoa ya kimila na Dick na sasa wanaishi kama mke na mume. “Ni kweli tumefunga ndoa ya kimila, tukachinjiwa mbuzi na kufanyiwa mambo ya mila ya upande wa mume wangu, ndoa ya kidini itakuwa ni sapraiz lakini kwa sasa sizungumzii tena mambo hayo,” alisema Shamsa

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname