MTOTO Junior Richard Rutta ambaye jinsi yake
haieleweki anatafuta msaada utakaomuwezesha kufanyiwa uchunguzi katika
hospitali ya CCBRT, jijini Dar es Salaam.
Mtoto huyo mwenye miaka miwili na miezi saba anaishi na mama yake mzazi, Sophia Kindamba, mtaa wa Mtwivilla, mjini Iringa.
Akiomba msaada huo, mama yake alisema jitihada za
madaktari wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuchunguza na hatimaye
kujua mtoto huyo ana jinsi gani zinaelekea kukwama.
“Kwa mara ya kwanza nilimpeleka katika hospitali
hiyo mwanzoni mwa mwaka 2012, lakini hadi hii leo hakuna majibu yoyote;
kwahiyo haieleweki kama ni msichana au ni mvulana” alisema huku machozi
yakimtoka.
Alisema mapema mwaka huu alikwenda Muhimbili
lakini kwa majibu aliyopewa amepoteza imani ya tatizo la mwanae
kushughulikiwa hospitalini hapo.
Kindamba alisema “nimeambiwa kipimo kile
kinatakiwa kupelekwa nje ya nchi baada ya uchunguzi wake hospitalini
hapo kushindikana.”
Alisema wakati akipewa majibu hayo ameshauriwa akajaribu pia kupata vipimo hivyo katika hospitali ya CCBRT.
“Nimerudi Iringa kutafuta hela ili nikienda CCRBT nisipate shida ya gharama za uchunguzi na matibabu,” alisema.
Kindamba alisema Katibu Tawala wa Wilaya ya
Iringa leo amempa barua itakayomuwezesha kupita kwa watu, taasisi na
mashirika mbalimbali kuomba mchango.
“Naomba mnichangie; baba wa mtoto
alinikimbi baada ya kubaini mtoto ana tatizo hili na sijui aliko; mimi
mwenyewe nashindwa kufanya biashara yangu ya kutembeza mitumba
kwasababu hali ya mtoto huyu sio nzuri,” alisema.
Alisema mtoto huyo huanguka na kupoteza fahamu
kwasababu ana tatizo lingine la mtindio wa ubungo lililogundulika katika
hospitali ya Muhimbili.
No comments:
Post a Comment