KESI YA KUFANYA MAPENZI NA MTOTO MDOGO WA KIGOGO YAWATESA BENZEMA NA RIBERY
Wachezaji soka wawili mashuhuri duniani wa timu ya taifa ya Ufaransa
wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la kufanya ngono
na kahaba aliyekuwa na umri mdogo Zahia Dehar .
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi alisema Franck
Ribery, mchezaji wa Bayern Munich alimtumia kama zawadi wakati wa
sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.
Inaripotiwa Ribery alimkatia msichana huyo tiketi ya ndege aweze
kusafiri kutoka Ujerumani mpaka Ufaransa kumtumbuiza wakati wa
kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo binti huyu anasema pia
alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema wa Real Madrid.
Benzema
amekanusha madai ya msichana huyu kwamba aliwahi kulipwa pia kufanya
nae ngono hotelini huko Paris wakati binti akiwa na umri wa miaka 16.
Ribery amekubali kwamba kweli alifanya ngono na msichana huyu kama
zawadi yake ya birthday lakini anasisitiza kwamba hakujua binti huyu
hakuwa amefikisha umri wa miaka 18.
Hawa wakali wa soka wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment