Wadau hapa nilipo nimechanganyikiwa na nisijue cha kufanya, naombeni
ushauri wenu, nilikwenda field huko Tabora, nikamwacha mchumba wangu
Tanga(ndiko kwetu) tulikuwa tukiwasiliana kama kawaida, na niliondoka
nikiwa nimeshavishwa pete.
Nilipigiwa simu baba yangu ni mgonjwa sana, watoto wake wote tulio
mbali, tunatakiwa kurudi Tanga, basi nami nilirudi, na kukuta kweli hali
ya baba si nzuri, nikampigia simu mchumba wangu kumuuliza yuko wapi,
ili tukutane nae hospitali, akasema kwamba amesafiri kikazi gafla kwa
siku moja tu then kesho yake angegeuza, nikamuuliza inakuwaje huniambii,
akasema nimesafiri gafla, hata hivyo nilitaka nikujulishe maana
nimeondoka leo.
Niliumia sana kwa alichokifanya, sasa kuna rafiki yangu mmoja
akaniambia, mbona mimi nimemuona jana super market? Akiwa na msichana?
Nilijisikia huzuni sana ila nilijipa moyo
nilikwenda moja kwa moja hadi kwake, nikamkuta mtoto wa mwenye nyumba,
nikamuuliza kama kweli mchumba wangu amesafiri,(nikajua labda alikwenda
supermarket kununua vitu vya safari) akasema mbona yupo? Na asubuhi
nimemuona?, nikampigia simu kuwa nipo pale kwake, akasema atachelewa
sana kurudi, hivyo nirudi nyumbani kesho ndio nije, nikamwambia
namsubiri, ilifika saa sita mimi niko mlangoni nimekaa namsubiri,
aliponikuta nimesinzia mlangoni alishtuka sna, na kuanza kunifokea
kwanini nisingesubiri hadi kesho.
Ile naingia tu! Ndani, nikakutana na sandols za kike, na kwenye mto kuna chupi ya kike, niliumia na kuanzisha ugomvi mkubwa,
Kinachonishangaza eti anasema yeye mwenyewe hajui ni vya nani, itakuwa
mama mwenye nyumba mchawi, maana alikuwa anamtaka, na bado anasisitiza
eti ananipenda na anataka nifunge nae ndoa mwezo wa tisa.
Sasa mimi hata sijui nifanyaje, naombeni ushauri wenu?
No comments:
Post a Comment